Jabazi sugu apata kichapo cha mbwa

0
5260
Mwizi aliyefumaniwa na kupewa kichapo karibu kufa na wakaazi wa Bondeni.

Siku za mwizi kweli ni arobaini, jabazi mmoja sugu aliye na mazoea ya kuwababaisha wanakijijini alinusurika kifo baada ya kufumaniwa na kupata kichapo cha mbwa kabla ya polisi kuwasili na kumwokoa kutoka kwa wanakijiji wenye hamaki.

Dakika chache alipokuwa akijaribu kufungua chumba kimoja, majirani waliskia na kupatwa na shauku kwamba hakuwa mwenye nyumba.

Punde tu walipomwona yule mwizi akaamua kukimbia lakini aende wapi? Wanakijiji wa Bondeni, Kitui walikuwa wamemzingira kila pembe huku wamebeba vifaa vyenye makali.

Hapo tu ndipo huyu jabazi akagundua kwamba siku zake arobaini zilikuwa zimewadia baada ya kuwaibia wakaazi wa Nehema na Talents kwa muda mrefu kila mara akitoroka kwa raha na madaha.

Wakazi wa Bondeni walisema kwamba mwizi yule sugu aliweza kutumia kifaa maarufu kama ‘master key’ hili kufungua na kupora mali ya wenzake mchana kutwa bila yeyote kujua.

Sasa yumo mwikononi mwa polisi huku uchunguzi ukiendelea. Wanakijiji wameonywa kukaa macho kila mara ili kujikinga na vitendo vya wezi waliomahiri kama yule.

ALSO READ:  Am set to liberate Machakos people - Katuku, Senatorial aspirant

Tarehe ishirini na nane Septemba,muda wa saa nne asubuhi ni siku atoisahau kamwe maishani mwake.

Facebook Comments