Mwanaume wa umri makamo ajitia kitanzi Kitui.

0
3115

Wakazi wa kata ya Waita iliyoko Kaunti ndogo ya Mwingi ya Kati katika jimbo la Kitui leo asubuhi waliamkia kisa cha kuhuzunisha baada ya kupata kimba cha maiti mwenye umri wa miaka 58 katika eneo lao.Kimba hicho kilipatikana kikining’inia kwa mti ulioko karibu na kituo kidogo cha kufanyia biashara cha Waita.

Akithimbitisha kisa hicho Chifu wa kata hiyo ya Waita Bwana Shadrach Wambua alisema ya kwamba mwili wa mwenda zake aliyebainika kwa jina Mutuku Mwaku ulipatikana ukining’inia kwa mti mapema asubuhi.
Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Waita wameanzisha uchunguzi kubaini kikamilifu chanzo cha kisa hicho.

Mwili wa mwendazake ulichukuliwa na maafisa wa polisi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Mwingi huku uchunguzi ukiendelea.
Kithembwa

Facebook Comments