Afueni kwa watahiniwa wa KCSE

  0
  1916

  Kulingana na takwimu idadi ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kitaifa KCSE imeweza kubainika kwamba zaidi ya wanafunzi 600,000 walishiriki zoezi la kufanya mtihani huo.Takwimu hizi ni kutoka wizara ya Elimu inayoongozwa na Waziri Dkt. Fred. Matiang’i.

  Idadi kubwa ya watahiniwa hawa wanatoka katika familia za mapato duni zisizojiweza.
  Hali hii ya umaskini inachangia wengi wao kulelewa mashinani kwa sababu za kifedha.

  Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 40 hawataweza kujiunga na vyuo vya kadri au vya mafunzo ya kiufundi angalau kwa kipindi cha mwaka mmoja ama kupata riziki.

  Njia mwafaka ya kuwasaidia watakaokosa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu vya umma ni kuwapa mafunzo ya kiteknolojia ya kisasa.

  Mafunzo haya yatawafaa katika ulimwengu wa leo wa kiteknolojia.Wengine wao hulazimika kutumikia jamii kwa kushiriki kufunza wenzao kuhusu utumizi wa kompyuta katika nyanja mbali mbali

  Mafunzo haya aghalabu hufanikishwa kwa kuandaliwa kwa warsha.Katika warsha hizi wanarika wengi hujifunza mambo mengi ya kiteknolojia ambayo hawakuyafahamu hapo awali.

  Kwa yeyote aliye na uwezo na ambaye angependa kujitolea kuwasaidia wanafunzi hawa anaweza kujisajili kupitia nambari ya usajili katika kibango kilicho juu.

  Kwa wasamaria wema walio na utu wa kuwasaidia wanafunzi hawa nafasi bado ingalipo.Kujisajili ni bure na hautozwi ada yoyote . Kujisajili bonyeza *384*2014*69# (Safaricom)
  Wito huu ni wa kuwasaidia wasiojiweza kutimiza ndoto zao.

  Facebook Comments