Mwanaume mmoja auawa Mwingi

0
2834

Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo hii leo ameuawa na wakazi wa kata ya Kavuvwani katika eneo bunge la Mwingi ya Kati.Maiti ya mwanaume mwenye umri wa kati leo umechukuliwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Mwingi na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Mwingi.

Mwanaume huyo alipoteza maisha yake baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wakazi waliokuwa na hasira nyingi. Wakazi hawa walighadhibika sana baada ya kugundua njama ya mwanaume huyo kumuibia na kumpiga sana mlevi mmoja.

Baadaye waliiteketeza maiti yake kwa moto.Akithimbitisha kisa hicho, Chifu wa Kavuvwani Bwana Mwinzi Muvengei alisema mwanaume huyo alitendewa kitendo hicho cha kinyama baada ya kumpiga mwenzake ambaye imesemekana kwamba alikuwa mlevi.

Yasemekana kwamba baadaye kijana huyo alimwibia pesa kiasi kisichojulikana jambo ambalo liliwakasirisha wakazi hawa kiasi cha kuchukua sheria mikononi. Mwanaume huyo anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Mwingi.Imesemekana alipata kuumizwa sana na kijana huyo.

Facebook Comments