Kesi inayopinga ushindi wa Mheshimiwa Nelson Musyoka kusikizwa.

0
2112

Kesi iliyowasilishwa katika mahakama moja kuu huko mjini kitui na aliyekuwa akiwania wadhifa wa uwakilishi Wadi wa Voo-Kyamatu Bwana Julius Kyale Muvio akipinga ushindi wa Mheshimiwa Nelson Musyoka Kivali ilisizwa  jummanne mwendo wa asubuhi.

Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama hiyo na aliyekuwa akigombea wadhifa huo na tikiti ya Wiper James Kyale kupinga ushindi wa Nelson Musyoka .

Mheshimiwa Nelson Musyoka alishinda kiti hicho akitumia chama cha Muungano katika uchaguzi mkuu wa 8/8/ 2017.Mashahidi wa Julius Kyale wanatarajiwa kutoa ushahidi wao hapo leo kuhusu dosari zilizokumba uchaguzi huo .Kikao hicho kinatarajiwa kuongozwa na jaji mkuu wa Mahakama ya Kitui Jaji Johnstone Munguti.

Kesi hiyo imepaniwa kusikizwa tena kwa kipindi cha siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 13/12/2017 hadi tarehe 15/12/2017 pale ambapo uamuzi wa mwisho utatolewa kuhalalisha ama kuharamisha uchaguzi.

Facebook Comments