Wafanyi biashara Mutomo walalamikia ukosefu wa stima.

  0
  1816

  Wafanya biashara katika soko la Mutomo lililoko Kitui Kusini wanalitaka shirika la usambazaji stima la KPLC tawi la Mutomo kushughulikia kwa haraka tatizo la stima.

  Wakiongea na waandishi wa habari, wafanya biashara hao wamesema kwamba stima imekuwa ikipotea mara kwa mara katika soko hilo.

  Jambo hilo wamelitaja kuathiri pakubwa biashara zao zinazotegemea sana stima.Wafanya biashara Wanaotumia jokofu kuhifadhi maziwa yasiharibike na wale wanaotumia stima kuchomelea milango na madirisha wameathirika pakubwa na tatizo hilo la ukosefu wa stima.

  Tatizo hilo wamelitaja kulemaza biashara zao wanazotegemea kama kitega uchumi chao.Wamesema kwamba wanakadiria hasara kubwa kutokana na tatizo hilo la kupoteapotea kwa stima katika soko hilo.

  Pia wameongeza kwamba huwa hawafahamishwi kuhusu kupotea kwa stima mara kwa mara katika soko hilo.Wameomba shirika la KPLC tawi la Mutomo kushughulikia tatizo hilo haraka iwezekanavyo.

  Wafanya biashara hao pia wameeleza kwamba iwapo tatizo hilo halitashughulikiwa kwa haraka ,watachukua hatua ya kushirikiana kwa pamoja na kuchanga pesa za kununua jenereta na kukoma kutegemea stima.

  Hii ni kwa sababu stima zikipotea huwa wanalazimika kutumia jenereta zao wenyewe jambo ambalo linawaletea hasara kubwa sana.

  Facebook Comments