Mwanamke mwenye umri wa makamo ajitia kitanzi Kitui.

0
2863

Wakazi wa kata ya Kithumula katika Wadi ya Mutonga-Kithumula eneo bunge la Kitui Magharibi Alhamisi ya leo 7/12/2017 waliamkia kisa cha kuhuzunisha.Hii ni baada ya kupata mwili wa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka kati ya 30-35 ukining’inia katika chumba alichokuwa amelala peke yake.

Ilisemekana mwanamke huyo alijinyonga usiku wa kuamkia leo nyumbani mwake kwa kutumia leso.Kisa hicho kilithimbitishwa na Chifu -Msaidizi wa kata-ndogo ya Kithumula Bwana Augustus Ngene.

Bwana Ngene alisema kuwa mwanamke huyo alikuwa mja mzito.Bwana Ngene aliongeza kwamba mwanamke huyo alijitoa uhai kutokana na tofauti na migogoro ya ndoa.Mwili wake ulichukuliwa na maafisa wa polisi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya Kitui.

Facebook Comments