Kesi inayopinga ushindi wa Ngilu Kusitishwa.

0
2957

Kesi iliyowasilishwa katika Mahakama kuu ya Kitui na Julius Malombe imehairishwa.Kesi hiyo ilikuwa isikizwe leo Alhamisi 7/12/2017.

Kesi hiyo iliwasilishwa na gavana mtangulizi wa Ngilu kupinga ushindi wake.

Kikao hicho kimehairishwa hadi tarehe 13/12/2017 ambapo kesi hiyo itasikizwa. Siku hiyo mashahidi wa Malombe watatakiwa kutoa ushahidi wao kuhusiana na kesi hiyo.

Kikao hicho kimesitishwa kutokana na Jaji Bi.Pauline Nyamwea kuwa mgonjwa kiasi cha kutofika kortini.

Hata hivyo, kesi ya uchaguzi inayomkabili mbunge wa Mwingi Kaskazini Mheshimiwa Paul Musyimi Nzengu imeendelea katika mahakama kuu ya Kitui. Mashahidi wa Nzengu walitoa ushahidi wao mbele ya jaji Mutende.

Kesi hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa mbunge wa Mwingi Kaskazini Mheshimiwa John Munuve.

Kikao hicho kiliongozwa na jaji Bi. Lilian Mutende. Kesi hiyo itachunguzwa kati ya tarehe 13/12/2017 -14/12/2017. Mwelekeo wa kesi hiyo utatolewa tarehe 9/1/2018 baada ya uchunguzi kukamilishwa.

Facebook Comments