Wazazi wa msichana aliyebakwa wataka haki kutendeka.

0
1903

Wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 14 kutoka kijiji cha Maiuni katika kata ya Kavaini huko Mwingi Magharibi wanataka haki itendeke kuhusu kubakwa kwa binti wao.Msichana huyo alibakwa na mfanyi kazi wao mwenye umri wa miaka 40.

Mwanaume huyo alikamatwa na maafisa wa polisi na baadaye kuachiliwa kwa njia zisizoeleweka.Kulingana na mama ya msichana huyo Christine Ndanu,msichana huyo alibakwa na mfanyi kazi wao wa nyumbani tarehe 21/11/2017.

Waliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Nguutani pamoja na kile cha Mwingi.Ameendelea kuelezea hasira zao kutokana na kuachiliwa kwa mshukiwa huyo na kutochukuliwa kwa hatua yoyote.

Christine amesema kwamba wamepata ripoti mbili kinzani kutokana na uchunguzi wa madaktari uliofanyika kubaini iwapo msichana huyo alibakwa au la.Uchunguzi kutoka hospitali kuu ya Mwingi unaonyesha kwamba msichana huyo hakubakwa ilhali uchunguzi uliofanyika katika hospitali ya Nairobi Womens Hospital unaonyesha kwamba msichana huyo alikuwa amebakwa.

Msichana huyo alieleza kuwa mfanyi kazi huyo aliingia chumbani alimokuwa akisoma.Msichana huyo alijaribu kujinusuru kutoka kwa mwanaume huyo ila akazidiwa nguvu na baadaye kutendewa kitendo hicho cha kinyama.

ALSO READ:  Kitui: County ministry procures fuel worth 12 million in a day

Christine amesema kwamba anaishuku sana ripoti ya uchunguzi kutoka hospitali ya Mwingi.Ameitaja ripoti hiyo kuingiliwa ili kuzuia kupatikana kwa matokeo ya kweli ili ushahidi ukosekane ndiposa mwanaume huyo aachiliwe huru.

Facebook Comments