Gavana Ngilu aendeleza miradi ya maji Miambani, Kitui.

0
2215

Ijumaa tarehe 8/12/2017,kikundi cha maafisa wa maji katika jimbo la Kitui walizuru kijiji cha Usiani kilicho katika wadi ya Miambani.Maafisa hao waliongozwa na Gavana Ngilu pamoja na mwakilishi wadi wa Miambani Mheshimiwa Alex Nganga.

Waliutembelea mlima wa Usiani ambao kwa sasa ni hifadhi kubwa ya maji.Gavana Ngilu na Nganga wamejitolea kuhakikisha kwamba wakazi wa Miambani wamepata maji safi ya kutosheleza mahitaji yao ya nyumbani,mifugo wao pamoja kunyunyizia mashamba yao ili kukuza mimea na mboga .

Unyunyiziaji mashamba ndio suluhu pekee itakayowezesha wakazi wa wadi kame ya Miambani na jimbo la Kitui kwa ujumla kuzalisha chakula cha kutosha.Hili litawasaidia pakubwa kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Facebook Comments