Gavana Ngilu kusisitiza Raila alimshinda Uhuru katika uchaguzi wa 8/8/2017.

0
1776

Gavana wa jimbo la Kitui Charity Ngilu Jumamosi tarehe 9/12/2017 alisisitiza kwamba kiongozi wa Muungano wa NASA Raila Odinga alimshinda rais aliye madarakani Mtukufu Uhuru Kenyatta.

Ngilu alisema hayo alipokuwa amehudhuria sherehe ya mazishi ya babake mmoja wa wabunge wa jimbo lake kutoka wadi ya Yatta-Kwa Vonza mheshimiwa John Mbaki Kisangau .

Aliongeza kwamba Rais Kenyatta alikosea pakubwa kwa kukubali kupokea kiapo cha kuliongoza taifa hili kwa muhula wa pili wa miaka mitano ilhali alijua wazi kwamba hakuwa ameshinda katika uchaguzi mkuu wa 8/8/2017.

Ngilu aliongeza kwamba wao kama viongozi wa upinzani wataendelea na juhudi zao za kumkumbusha Rais Kenyatta kwamba alishindwa na kiongozi wa upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita.

Facebook Comments