Kitui: Msichana aliyetaka kujiua atiwa mbaroni

0
2148

Msichana mwenye umri wa miaka 15 kwa sasa ako chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi katika jimbo-ndogo la Matinyani eneo bunge la Kitui Magharibi.

Jumatatu ya leo tarehe 11/12/2017, maafisa wa polisi kutoka jimbo-ndogo la Matinyani walimtia nguvuni msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 kwa kitendo cha kutaka kujitoa uhai.

Imeripotiwa kwamba msichana huyo kutoka kata ya Mutonga alikunywa sumu Ijumaa ya tarehe 9/12/2017 huku akikusudia kujitoa uhai.

Kulingana na Kamanda wa polisi wa jimbo-ndogo la Matiny’ani Isaac Kiragu, msichana huyo alichukua hatua hiyo baada ya kunyimwa nafasi ya kuenda jijini Nairobi kumsalimia ami yake.

Kamanda huyo wa polisi ameongeza kwamba msichana huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya kibinafsi ya Neema mjini Kitui.

Msichana huyo anatarajiwa kufikishwa mahakama ya Kitui baada ya kupata afueni na kushtakiwa kesi ya kutaka kujitoa uhai.Atashtakiwa chini ya sheria za watoto.

Facebook Comments
ALSO READ:  Kitui: County ministry procures fuel worth 12 million in a day