Gavana Ngilu kulalamikia masaibu wanayopitia Wakenya wakati wa sikukuu ya Jamhuri.

0
2654
Profile Photo: Kitui Governor, Hon Charity Ngilu

Gavana Ngilu alikaidi wito wa kujumuika pamoja na kusherehekea sikukuu ya Jamhuri iliyofanyika tarehe 12/12/2017.Sikukuu hiyo huadhimishwa kila mwaka kukumbuka wakati taifa letu tukufu la Kenya lilipata uhuru wa kujitawala lenyewe na wabeberu.

Gavana Ngilu alitumia fursa hiyo kuzuru maeneo tofauti katika jimbo lake kujionea jisnsi ukuzaji wa chakula ulivyo katika mashamba ya wakulima pamoja na kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja na wao kuhusu jinsi ya kuliendeleza jimbo la Kitui mbele.

Akizungumza na wakazi wa maeneo ya Nzambani,Kisasi pamoja na Mbitini, Gavana huyo alisema kiwango duni cha miundo msingi kama vile afya duni,barabara mbovu na uhaba wa maji ndizo zastahili kupewa kipaumbele kuliko sherehe ya Jamhuri.

Gavana Ngilu alilalamikia matumizi ya pesa nyingi kugharamia sherehe hiyo ilhali Wakenya wa kawaida wanazidi kuzongwa na kusakamwa na umaskini,magonjwa na maendeleo duni.

“Sioni haja ya kujiunga pamoja kusherehekea sikukuu ya Jamhuri ilhali watu wangu wanakandamizwa na magonjwa,umaskini ,afya duni na maisha ya kiwango cha chini kabisa.Viongozi waliochaguliwa wamepuuza maslahi ya Mwananchi wa kawaida,” Gavana Ngilu alisema.

ALSO READ:  Kitui: County ministry procures fuel worth 12 million in a day

Gavana huyo pia alizungumzia njia mbalimbali serikali yake itatumia ili kuendeleza maisha ya wakazi wa jimbo lake.Aliwarai Wawakilishi Wadi kuipitisha miswada ya ustawishaji wa maendeleo katika jimbo hilo ili kutimiza ahadi alizowaahidi wapiga kura wa Kitui wakati wa kampeni.

“Leo niko na furaha nyingi sana kuona Wawakilishi Wadi wengi hapa.Nawaomba waweze kuniunga mkono kikamilifu katika kuwatumikia watu wa Kitui,” Gavana ngilu aliongeza katika usemi wake.

Ngilu pia aliwaomba Wawakilishi wadi kutenga kiasi kikubwa cha bajeti kitumike kufanikisha miradi ya maji ili kusaidia katika kilimo cha kisasa ili kuzalisha chakula cha kutosha.Mbali na hayo,aliomba umoja wa viongozi waliochaguliwa ili kushirikiana pamoja kukabiliana na umaskini.

Pia aliomba serikali kuu ya kitaifa kuwatumikia Wakenya wote kwa usawa ili kufanikisha maendeleo vijijini.

“Uongozi wa taifa letu umeshindwa kuwatumikia Wakenya kikamilifu.Lazima tumalize umaskini katika taifa letu na tuonyeshe uongozi wa kweli,” alisema Ngilu.

Wengine waliondamana na Ngilu ni naibu wake Dr. Wathe Nzau ambaye aliunga mkono usemi wa gavana Ngilu kuhusu kukabiliana na umaskini pamoja na kuinua kiwango cha maisha cha wakazi wa kitui.

ALSO READ:  Kitui: County ministry procures fuel worth 12 million in a day

Naibu Spika wa bunge la jimbo la Kitui,Mheshimiwa Kasee Musya ambaye pia aliandamana na Ngilu alisema kwamba atawashinikiza Wawakilishi Wadi kupitisha miswada inayolenga maslahi ya wakazi wa Kitui moja kwa moja ili kuwanufai.

Facebook Comments