Mwanaume mmoja kufa baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani

0
3539

Mwendeshaji mmoja wa bodaboda ameripotiwa kufa papo kwa hapo baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani Mwingi jimbo la Kitui.Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatano tarehe 13/12/2017.Ajali hiyo ilihusisha pikipiki moja na gari moja la kibinafsi katika barabara kuu ya Thika kuelekea Mwingi karibu na soko la Nguutani.

Imeripotiwa kwamba gari hilo liligongana ana kwa ana na mwendeshaji huyo wa bodaboda katika kizuizi cha barabarani katika barabara ya kuelekea soko la Nguutani.Ajali hiyo ilithimbitishwa na Mkuu wa Polisi wa Migwani Julius Muu ambaye akizungumza na wanahabari alisema mwendeshaji bodaboda huyo alikuwa anatoka Nzawa ilhali gari hilo lilikuwa linatoka pande za Kithyoko katika jimbo la Machakos.

Julius Muu alisema maiti ya mwanaume huyo ilichukuliwa na maafisa wa polisi wa kituo cha Mwingi na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya Mwingi.Aliongeza kwamba dereva wa gari hilo alipata maumivu na anaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya serikali ya Mwingi.

Facebook Comments