Kamishna wa Kitui kuwahakikishia wakazi kupata hati miliki bila malipo.

0
2645

Kamishna wa Kitui Boaz Cherotich aliwahakikishia wakazi wa jimbo hilo kwamba serikali kuu ya kitaifa itawapatia hati miliki za mashamba bila malipo.Akizungumza Jumanne ya leo 13/12/2017 alipokuwa katika soko la Zombe eneo bunge la Kitui Mashariki/Mutito,Cherotich alisema ya kwamba serikali kuu ya kitaifa iko tayari kuhakikisha kila mkazi wa Kitui amepata hati miliki kwa njia halali ,ya uwazi na kwa usawa.

Kamishna Cherotich alisema ni jambo la kuhuzunisha kuona wananchi wakitozwa ada ya kiasi fulani cha pesa ili wapate hati miliki hizo.Kamishina huyo aliongeza kwamba hati miliki zaidi ya elfu 100 ziko tayari na kuwaomba wakazi wa Kitui kufika katika ofisi za usajili wa mashamba na kuzichukua haraka iwezekanavyo.

Facebook Comments