Vurugu kuzuka katika Mahakama Kuu.

0
2732

Shughuli za mahakama zilitatizika leo Alhamisi tarehe 14/12/2017 katika Mahakama Kuu ya Milimani.

Usalama kwa sasa umeimarishwa na maafisa wa polisi ndani na nje ya majengo ya Mahakama Kuu ya Milimani jijini Nairobi baada ya vurumai kuzuka wakati wa kusikizwa kwa kesi iliyowasilishwa na Malombe kupinga ushindi wa Gavana Ngilu.

Hii ni kutokana na wafuasi wa aliyekuwa gavana wa Kitui Julius Malombe kuzua vurugu katika korti hiyo.Kizaazaa hicho kilisababisha Jaji Bi. Nyamweya kusitisha kikao hicho kwa muda.

Katika kisanga hicho wafuasi kadhaa walitiwa nguvuni na maafisa wa polisi wakiwemo wanawe wawili wa Malombe.

Jaji Bi.Nyamweya alilazimika kuamrisha kikao hicho kuendelea bila wafuasi wa mshtaki na mshtakiwa.

Facebook Comments