Meneja wa Equity tawi la Mwingi ajipata taabani.

0
3703

Mbunge wa Mwingi ya Kati Mheshimiwa Gideon Mulyungi kumkashifu vikali Meneja wa benki la Equity tawi la Mwingi.Hili ni kutokana na tendo la Meneja huyo kuwa akiwaitisha hongo wazazi ili kuwasajili watoto wao katika mpango wa kuelimisha watoto kutoka familia zisizojiweza almaarufu Wings to Fly unaofadhiliwa na benki la Equity.

Mbunge huyo alisema kwamba amekuwa akipata malalamishi mengi katika ofisi yake kutoka kwa wakazi wa Mwingi kuhusu mpango huo unavyoendeshwa.Amesisitiza kuwepo haja ya viongozi wote kushirikishwa katika zoezi hilo kama njia moja wapo ya kuhakikisha mpango huo umezaa matunda.

Isitoshe,aliezeza kwamba yeye kama kiongozi anajua wazi masaibu wanayopitia wakazi wa eneo bunge lake na kwamba amekuwa akiwafadhili watoto kutoka familia maskini kielimu ili kutimiza ndoto zao.

Mulyungi alimlaumu Meneja huyo kwa kutozingatia usawa na ukweli katika zoezi hilo.Mbunge huyo pia alimuonya Meneja huyo kukomesha tendo hilo potovu haraka iwezekanavyo na kuwahusisha viongozi waliochaguliwa kikamilifu katika zoezi hilo la sivyo hatua kali za kiserikali zichukuliwe dhidi yake.

Facebook Comments
ALSO READ:  Kitui: County ministry procures fuel worth 12 million in a day