Serikali ya Gavana Ngilu kutapeliwa

0
3160

Gavana Malombe kuendelea kupata marupurupu kutoka kwa serikali ya Kitui licha ya kubanduliwa mamlakani na Gavana wa sasa Charity Ngilu.

Imesemekana kuwa Gavana huyo wa zamani amekuwa akipokea marupurupu ya shilingi 400,000 kila mwezi kutoka kwa serikali ya jimbo la Kitui tangu mwezi wa Agosti baada ya uchaguzi mkuu.
Kwa sasa amesemekana kuwa amepokea zaidi ya shilingi 2 Milioni kufikia wiki ya kwanza ya Disemba wakati uozo huo ulifichuliwa.

Kulingana na wandani wa kisiri wa Kitui Online,fedha hizo zimekuwa zikitumwa kwa Gavana huyo kupitia kwa wakala fulani wa kaunti ambaye alikuwa akizipokea kutoka kwa afisa fulani ambaye kwa sasa hajabainika wazi.

Uozo huo ulifichuliwa kwa maafisa wa Ngilu na afisa mmoja ambaye jina lake limebanwa kwa sababu za kiusalama.Afisa huyo alizipata taarifa hizo kupitia kwa mazungumzo yaliyohusisha maafisa wa fedha wa jimbo hilo na hapo baadaye kuwadokezea maafisa wa Ngilu.

Kwa sasa malipo hayo yamesitishwa na inakisiwa kwamba mhusika mkuu katika kashfa hiyo ni mmoja kati ya maafisa wakuu wa jimbo ambaye alienda likizoni kati ya mwezi wa Oktoba na Novemba.

Facebook Comments