Mfanyi biashara tajika kuwaacha wakazi wa Mwingi vinywa wazi.

0
5252

Mfanyi biashara mashuhuri kutoka jijini Nairobi bwana Henry Waswa alikishtua kijiji cha Nzatani katika Mwingi Magharibi baada ya kutua na helikopta akiandamana na wabunge kadhaa siku ya Jumamosi katika sherehe ya kulipa mahari ya Moreen Tabitha.

Magari ya kifahari yalikuwa yamepangwa pembeni na kurembeshwa kwa maua ya kila sampuli tayari kuwalaki wageni hao.Bwana harusi aliandamana na wabunge kadhaa akiwemo mbunge wa eneo hilo la Mwingi Magharibi Mheshimiwa Charles Nguna,Mh.Babu owino wa Embakasi Mashariki,Mh.Caleb Hamisi wa Sabot pamoja na Mh. Alfred Keter wa Nandi Hills.

Hafla hiyo iligharimu mfanyi biashara huyo mzaliwa wa jimbo la Bungoma zaidi ya shilingi milioni 5 . Pia, imebainika kwamba wana ndoa hao walibadilishana pete zenye thamani ya shilingi 1.6 milioni pesa za Kenya.

Watumbuizaji wa muziki pia walijizolea kiasi fulani cha pesa akiwemo mwimbaji maarufu kutoka ukanda wa Ukambani Ken Wa Maria ambaye inakisiwa kwamba alipata takriban laki 3 huku msanii T Broz Africa kutoka Kitui shilingi laki 2.5.

ALSO READ:  Kitui: County ministry procures fuel worth 12 million in a day

Kijana mcheshi kutoka Church Hill Show,Chipukeezy ndiye alikuwa mwenye sherehe katika hafla hiyo.Mcheshi huyo Kutoka Churchill alipata shilingi 150,000.Msanii wa nyimbo za injili Justus Myelo na Kikundi cha Luhya pia walikuwepo kuwatumbuiza wanasherehe.

Ulinzi mkali ulikuwa umeimarishwa na maafisa wa polisi katika boma hilo .Hata hivyo,haikuwekwa wazi kiasi cha pesa kilichochangishwa siku hiyo.Baada ya sherehe hiyo, wana ndoa walisafiri nchi za ng’ambo ili kufunga pingu za maisha.Haijawekwa wazi walipo.

Facebook Comments