Wakazi wa Mutha kuomba serikali kuu kuwimarishia ulinzi.

0
1359

Wakazi wa Mutha katika gatuzi la Kitui kuielekezea kidole cha lawama serikali ya kati kupitia Wizara ya Masuala ya Ndani na Uratibu kwa kulegeza juhudi zao kupambana na wafugaji wa ngamia kutoka jimbo jirani la Tana River.

Wakazi hao kutoka sehemu tofauti katika eneo bunge la Kitui Kusini wamesema kuwa jamii ya Somali imekuwa ikiwashambulia mara kwa mara na kutekeleza mauaji,kuchoma nyumba zao pamoja kulisha ngamia katika mashamba yao jambo ambalo limewasababishia hasara kubwa sana.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kalia Katune katika kata ya Ndakaini amewaambia wanahabari kwamba wafugaji hawa wametoroka makwao na kuhamia sehemu tofauti katika Kitui huku wakiandamana ngamia na mbuzi zaidi ya 500 na kuwalisha mifugo hao katika mashamba yao.

Baadhi ya wafugaji hawa wanasemekana kuwa wamekodi nyumba katika soko la Mutha na kuanzisha biashara za duka na kufungua hoteli mbalimbali.Wengine wao wanalaumiwa kwa kitendo cha kuwa wakijenga nyumba za manyatta katika boma za wenyewe bila makubaliano rasmi jambo ambalo linawazidishia hofu ya usalama wao.

Imesemekana kwamba wafugaji wengine wamenunua magari ya kuwawezesha kuzuru maeneo tofauti katika wilaya hiyo.

Kwa sasa wakazi hawa wanaiomba serikali kuu kuingilia kati na kushughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo na kuwaokoa.

Mkazi mmoja amesema kwamba wamekuwa wakipiga ripoti kwa Machifu wa eneo hilo ambao wamekuwa wakiwachukulia hatua za kiserikali wafugaji hawa.

Facebook Comments