Mlanguzi wa bangi kufikishwa Mahakamani Kitui.

0
1828

Mwanaume mmoja mwenye umri mpevu alifikishwa katika mahakama moja mjini Kitui kwa kosa la kupatikana na kilo 3 unusu za bangi.

Mwanaume huyo alifumaniwa nyumbani mwake na bangi hiyo yenye thamani ya shilingi 3,600 katika makazi yake rasmi sehemu ya Mjini viungani mwa mji wa Kitui tarehe 23 Desemba,2017.

Mbele ya jaji Bi. Maryanne Murage, mshukiwa huyo kwa jina Solomon Mwololo alikana madai hayo ya uraibu wa bangi na kutakiwa kulipa bondi ya shilingi 50,000 pesa taslimu au mthamini wa kiasi hicho ili aachiliwe huru kesi iwe ikisikizwa akiwa nje.

Kesi hiyo itasikizwa tena tarehe 10Januari,2017 na tena 24 Mei,2017.

Facebook Comments