Sinyoi mpaka Baba “aapishwe,” Msanii Katombi.

0
3462

Mwimbaji maarufu kutoka ukanda wa Ukambani kwa jina la kiusanii Katombi aliwaacha wafuasi wake katika hali tatanishi baada kuandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba hatanyoa nywele zake hadi pale Baba “ataapishwa” na kuwa “rais wa Jamhuri ya Wakenya”

Taarifa hizo ziliibua hisia mseto na kinzani baina ya mashabiki wake sugu.Baadhi wanamtazamia kuwa mbunifu zaidi ili kuwafurahisha mashabiki ilhali wengine wanamtazama tu kama msanii aliyewajibika kama kawaida katika jukumu alilojitwika.

Utata umesalia ni kipi kilichomsukuma msanii huyo kuyataja mambo yanayohusu siasa jambo ambalo ni nadra sana kwa wasanii .Hii ni kwa sababu wasanii hukwepa masuala ambayo yanaweza kuleta hali tatanishi,udhalalishaji au hata mgawanyiko baina ya wafuasi wao hasa masuala ya siasa.

Facebook Comments