Uteuzi wa Wings to Fly kwa wasomi kukamilika Kitui

0
1568

Wanafunzi 8 kutoka eneo bunge la Mwingi katika jimbo la Kitui wamepata ufadhili kutoka benki la Equity tawi la Mwingi .Mpango huo ulikamilishwa hapo jana Alhamisi tarehe 28/12/2017.

Mpango huo wa elimu kwa wanafunzi wenye wazazi wasiojiweza kiuchumi wa benki la Equity almaarufu Wings to Fly ulianzishwa mwaka wa 2010.Kufikia sasa takriban wanafunzi 1000 kutoka familia zisizojiweza wamenufaika na mpango huo kote nchini Kenya tangu kuanzishwa.

Akizungumza katika zoezi hilo Mjini Mwingi, Naibu Gavana wa Kitui Mh. Dkt. Wathe Nzau aliongeza kwamba serikali ya Kitui itatenga kiwango fulani cha hela ili kutoa ufadhili zaidi kwa wanafunzi kutoka familia zisizojimudu kiuchumi kupata elimu .Jambo hilo litawezesha wanafunzi hao kutimiza ndoto zao za siku za usoni.

Naibu Gavana huyo aliongeza kwamba serikali ya gatuzi la Kitui itatenga shilingi milioni mbili kwa kila wadi ili kufanikisha mipango ya elimu.

Zoezi kama hilo liliendeshwa katika eneo bunge la Kitui ya Kati huku likiongozwa na Waziri wa Elimu wa Kitui Mh. David Kivoto.Katika shughuli hiyo wanafunzi 8 walisaidika kutokanana na mpango huo.

Waziri huyo aliirai benki ya Equity kutenga kiwango zaidi kuwezesha watoto wengi kupata elimu bora.

Facebook Comments