Mbunge wa Mwingi kuiomba serikali ya Jubilee kutekeleza mpango wa Elimu bila malipo

0
1493
Hon. Gideon Mulyungi, Mwingi Central MP

Mbunge wa Mwingi ya Kati katika gatuzi la Kitui Mheshimiwa Gideon Mulyungi hapo jana Jumanne 2 Januari, 2018 alimuomba Mtukufu Rais Uhuru Kenyatta kutimiza ahadi ya elimu bila malipo kwa shule za upili.

Rais Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto waliahidi Wakenya kuanzisha na kutekeleza ahadi yao ya elimu bila malipo pindi watakapochaguliwa Kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Fred Matiang’i alisema kwamba serikali ya Jubilee chini ya uongozi wa Kenyatta na Ruto iko tayari kutekeleza mpango huo wa elimu bila malipo.Aliongeza kwamba ni haki ya kila mwanafunzi wa Kenya kupata elimu bora kwa gharama ya chini.

Rais Kenyatta na naibu wake waliahidi Wakenya kutekeleza mpango wa elimu bila malipo wakati wa kujitafutia umaarufu na uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8,2017.

Mheshimiwa Dkt. Mulyungi aliyasema hayo akiwa nyumbani mwake huko Kalisasi wilaya ya Mwingi alipokuwa akituma ujumbe na salamu za mwaka mpya kwa wakaazi wa eneo bunge lake na Wakenya wote kwa jumla.

Aliongeza kwamba amepata barua zaidi ya 30 katika ofisi yake kutoka kwa wazazi na wanafunzi mbalimbali kuwafadhili kifedha ili waweze kujiunga na kidato cha kwanza hivyo basi kuomba serikali kuingilia kati na kutatua utata uliopo ili wanafunzi kutoka familia zenye mapato ya chini wanufaike na mradi huo.

Facebook Comments