Wapinzani wakuu wa Ngilu kutumia Propaganda kumkashifu.

0
1914

Wapinzani wa Gavana Ngilu wa kisiasa wamebadili mkondo wa siasa zao na kuwa za ulaghai na uwongo unaolenga kuwapotosha wafuasi wake kwa kupuuza utenda kazi wake.Utenda kazi wake umepakwa tope si haba na wapinzani wake wakuu walio na nia ya kumharibia sifa mbele ya mpiga kura.

Hata hivyo,Kila mkaazi wa jimbo la Kitui anapinga na kutofautiana vikali na uvumi unaosambazwa na anayefahamika kwa jina la utani kama “Tharaka”.Huyu agenda yake kuu imebainika wazi kuwa ni kupotisha wafuasi wa Gavana Ngilu.

Huyu ” Tharaka” analenga kuwapotosha watu wa Kitui kwa kuikashifu vikali serikali ya Gavana Ngilu na kusingizia kwamba Ngilu anaiendesha serikali ya Kitui kama familia ya mtu binafsi.Huo anauona uongozi usiofaa kwa watu wa Kitui na nchi kwa jumla

Tangu kuapishwa kwake kama Gavana wa Not pili wa gatuzi la Kitui,Ngilu amekuwa akiwashirikisha wakaazi wa Kitui katika uongozi wake kwa njia mbalimbali.Wapiga kura wamekuwa wakihusishwa katika mipango ya maendeleo kikamilifu.

La hivi karibuni ni mradi wa uzalishaji chakula ulioanzishwa na Gavana ngilu pindi alipochukua hatamu ya uongozi kwa muhula Wake wa kwanza wa miaka 5 kama gavana almaarufu Ndengu Revolution.Mahasimu wake wa kisiasa wanautumia mradi huo kujinyakulia sifa za kuwa viongozi bora na wanaofaa.

Wanaulaumu mradi huo kwa kutofaulu kwake jambo ambalo limesababishwa na ukosefu wa mvua ya kutosha.Hata ingawa mazao yaliyotarajiwa hayatapatikana kwa sababu ya ukosefu wa mvua tisha,wakulima bado watavuna mazao kidogo yatakayowawezesha kukimu mahitaji yao ya chakula na hela.

 

Thoughts expressed are those of the contributor and do not necessarily represent the views of KO

Facebook Comments Box