Nyoka mwenye pete tumboni kuonekana Maliku, Kitui.

0
4239

Wanakijiji wa Kikuuni kuona maajabu jana Jumatano tarehe 4/01/2018 baada ya nyoka kuonekana na pete katika boma la Kitema Kikonde .

Kulingana na Chifu wa kata hiyo ya Maliku Bw. Julius Mwendwa Munyaka ni kwamba nyoka huyo aliuawa na kuchomwa na wanakijiji waliokuwa wamejawa na wahka baada kupokea amri kutoka kwa Kasisi mmoja anayehudumu katika eneo hilo.Baada ya kushindwa la kufanya,wanakijiji walipigia Mhubiri huyo simu na kuwaagiza waiue na kuichoma nyoka hiyo wakiwa na imani tele.

Agizo hilo la Kasisi huyo liliwatia moyo na kuwapa nguvu na ushujaa wa kukabiliana vikali na “shetani” huyo.Baada ya kuua nyoka huyo,walimteketeza kwa moto lakini pete iliyokuwa mwilini mwake ikabakia kwani ilikuwa ya chuma.

Chifu huyo aliongeza kwamba wakati wa mazishi ya mwenye boma hilo mwendazake Kitema Kikonde takriban wiki mbili zimepita mnyama fulani ambaye hakubainika wazi alianguka kutoka juu ya mti na kumtatiza mwanawe marehemu kabla ya kuuawa na watu.

Mkewe mwenda zake Jacinta Kasyima Kitema alisema kwamba walisikia kuku wakiteta mwendo wa saa kumi alasiri na kuiua kwa kutumia kipande cha mti alipomwona nyoka huyo.

Aliporudi kutoka chumbani mwake alipata nyoka huyo amefufuka na alipokuwa akitaka kumuua tena nyoka huyo ndipo aliona pete ya chuma iliyokuwa tumboni mwake jambo lililokatiza juhudi zake za kumuangamiza nyoka huyo.

Pia mjane huyo alisema nyoka huyo alitokea upande wa kaburi la mumewe ila alipoenda hapo hakuona shimo lolote.

Facebook Comments