Pwani lazima ijitenge na Kenya, asisitiza gavana Kingi

0
2272

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jeffwa Kingi amesisitiza kuwa mipango ya kuzitenganisha kaunti za pwani na taifa la Kenya bado yaendelea kama awali.

Akitoa hotuba ya gavana  katika kaunti ya Kilifi, Bw. Kingi ametilia mkazo kuwa serikali kuu imeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa kaunti za pwani na katika ugavi wa hela.

“Tulipopata katiba mpya mwaka 2010, tulidhani kuwa mambo yatatuendea sawa pwani.Lakini sasa ikiwa katiba hii haifanyi kazi, ikiwa hata na katiba hii wazi lazima tupige magoti kule Nairobi kuomba pesa, basi kujitenga kwa pwani ni jambo la lazima.” Alilalama gavana Kingi.

Kingi alizidi na kuishutumu serikali kuu akisema kuwa majukumu ya serikali za kaunti sasa yanatekelezwa na serikali ya kitaifa pamoja na serikali za kaunti kutopokea pesa ambazo zinafaa kutumika katika miradi ya maendeleo ya kaunti.

“Huu mlio wa kwamba tunataka tujitenge hauletwi na wapwani. Unaletwa na kutowajibika kwa serikali ya kitaifa. Wangetekeleza katiba vile ilvyo, hakuna mpwani hata mmoja angesimama akalia.Lakini kabla ya katiba tulikuwa tunalia, baada ya kupata katiba mpya tukadhani tutapata afueni kidogo, lakini ni kama kutoka kwenye kaango kuangukia makaa yenye moto.” Kingi alidai.

Facebook Comments