Wafanyi Biashara Makueni kukadiria hasara kubwa baada ya vioski kubomolewa

0
2081

Wafanyi biashara wa kaunti ya Makueni katika soko la Salama kando ya barabara kuu ya kuelekea jijini Mombasa kuamkia jambo la kuhuzunisha baada ya kupata vioski na vibanda vyao vimebomolewa na shirika la ujenzi na upanuzi wa barabara Kenya la Kenya National Highways Authority,KENHA.

Wafanyi biashara wanaoendeleza biashara ndogo ndogo kando ya barabara kuu ya Nairobi kuekekea jijini Mombasa katika kituo kidogo cha kibiashara cha Salama katika gatuzi la Makueni wanaendelea kuhesabu gharama baada ya kuamka asubuhi na kupata kioski zao zimebimolewa.

Shirika la ujenzi na upanuzi wa barabara kuu hapa nchini kenya la KENHA usiku wa kuamkia leo liliendeleza shughuli hiyo ya ubomoaji wa vioski na vibanda vilivyojengwa karibu na barabara hiyo.

Vibanda hivyo vyasemekana kujengwa karibu sana na barabara hiyo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa binadamu.Hii ni kutokana na magari mengi yanayopita barabara hiyo kwa mwendo wa kasi.Hata hivyo,vioski hivyo vyasemekana kujengwa hapo kinyume cha sheria kwani sehemu hiyo ilihifadhiwa upanuzi wa barabara hiyo.

ALSO READ:  Makueni based lawyer succumbed to the injuries

Wafanyi biashara hao kwa sasa wanalaumu KENHA kwa kutekeleza hayo bila kuwatahadharisha awali ili watoe kioski zao pamoja na mali yao karibu na barabara hiyo. Pia wanateta kwamba mali yao yenye thamani kubwa ambayo imeharibiwa ndani ya vibanda hivyo.Wengi wao biashara hizo zilikuwa kitega uchumi chao na kwa sasa hawana njia mbadala ya kuendesha maisha yao.

Mali ya thamani isiyojulikana iliharibiwa wakati wa zoezi hilo.Wafanyi biashara hao hawakulipokea jambo hilo kwa furaha kutokana na uharibifu mkubwa wa mali ulioendelezwa wakati wa zoezi la kubomoa vibanda hivyo.

Facebook Comments