Utata kuibuka kuhusu msanii mkongwe Ancent Munyambu.

0
2314

By Kiriba

Habari za Kushangaza kuibuka kuhusu nyimbo za Mwanamuziki Munyambu.

Siku chache baada ya kifo cha mwanamuziki maarufu wa nyimbo za kale za Kikamba Ancent Munyambu sasa habari zimeibuka kwamba msanii Boscow Mulwa ndiye aliyeimba nyimbo zinazojulikana na kuaminika kuwa za Munyambu.

Mashabiki wao sasa wamepata kujua ukweli uliopo baina ya wasanii hao wawili.Hata hivyo,wasanii hao walibakia marafiki wakuu hadi kifo cha Ancent Munyambu.

Munyambu husemekana kuwa ndiye aliyeimba nyimbo maarufu kama vile “kavola kamengele” na “sili sya ma cow-boy.” Kulingana na mahojiano ya moja kwa moja katika runinga ya Kikamba ya Kyeni TV na DJ Biado Mulwa alisema nyimbo hizo ndiye aliyezitunga na kuziimba wa kwanza.

Aidha,ukweli zaidi uliibuliwa na kanda ya video iliyowekwa mitandaoni ya kijamii tarehe 05/01/2018, ambapo Bosco Mulwa alisema kwamba ndiye aliyeimba nyimbo hizo kwa ushirikiano na Francis Danger.

Mulwa aliongeza kwamba hakuona haja yoyote ya kwenda mahakamani na kumshtaki rafiki huyo wake wa zamani na pia msanii mwenzake.

Kinaya ni kwamba Munyambu ndiye aliyemwambia babake Bosco Mulwa kwamba mwanawe Bosco alikuwa na kipawa cha uimbaji.

Kwa sasa Mulwa ndiye msanii mashuhuri wa zamani aliye hai katika ukanda wa Ukambani.

Nyimbo za Mulwa zilizotia fora ni kama vile mother na “kwitu Makueni.”

Facebook Comments