Malumbano kuibuka baina ya Msemaji wa Naibu Rais na Mwanahabari Nation.

0
1470

David Mugonyi,ambaye ndiye msemaji mkuu wa Naibu Rais Mtukufu William Ruto alizozana kwa simu tamba na mwanahabari wa Nation Justus Wanga kuhusu Baraza mpya la Mawaziri lililotangazwa siku chache zilizipita na Rais wa Jamhuri tukufu la Kenya Mtukufu Uhuru Kenyatta.

Hali ya utata kuhusu hatima ya baadhi ya na mawaziri ambao Kenyatta hakuwataja katika awamu ya ya kwanza iliweza kuzua hofu na sitifahamu baina ya Wakenya wengi.

Wahka huu ulichangiwa na kutokuweko kwa baadhi ya majina ya mawaziri wa sasa katika orodha ya kwanza aliyoidoma Rais Kenyatta.

Katika kanda iliyorekodiwa,hao wawili walinaswa wakizozana kuhusu orodha ya Baraza mpya la Mawaziri la Rais Kenyatta.Wanazozania kutokuweko kwa baadhi ya majina ila Msemaji Naibu Rais ashikilia ni hadi pale orodha nzima itatangazwa ambapo itabainika kama kuna waziri ametimuliwa au la.

Rais anatarajiwa kuisoma orodha yote ya Baraza lake la Mawaziri wiki hii.

Facebook Comments