Kitui: Mama Kushtakiwa Kumuuza Mwanawe.

0
2017

Wanawake wawili wenye umri kati ya miaka 25-30 Jumatatu ya leo 08 Januari, 2017 walifikishwa mahakama mjini Kitui kwa kosa la kuendeleza biashara ya kuuza mtoto mdogo.

Mnamo tarehe 1 Januari, 2018 katika soko la Kanyangi eneo bunge la Kitui Rural,wanawake hawa kwa majina Sarahi Kwamboka na mwenzake Bentete Musengy’a walifumaniwa walipokuwa wakiendeleza biashara hiyo. Wakaazi wa eneo hilo waliwadokezea kisiri maafisa wa kituo kidogo cha polisi wa utawala cha Kanyangi ambao hapo baadaye walianzisha msako wa kuwanasa hawa wawili.

Maafisa wa polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni wahalifu hao wawili siku moja baada ya kuanzisha msako wa kuwatafuta. Mteja wa Sarahi Kwamboka,Benteta Musengy’a alikuwa amnunue malaika huyo mwenye umri wa siku 3 kwa bei ya 10,000 pesa taslimu za Kenya.

Hawa wawili walikiri makosa yao mbele ya hakimu wa mahakama ya Kitui Johnstone Munguti. Kesi hiyo itasikizwa tena tarehe 18 Januari, 2018 baada ya korti hiyo kupata ripoti kamili kutoka kwa afisa mkuu wa masuala ya watoto kuhusu hatima ya mtoto huyo mchanga.

Mama mzazi wa kitoto hicho kichanga Sarahi Kwamboka aliweka bayana kwamba alichukua hatua ya kumuuza mtoto wake kwa vile hangemudu kusimamia malezi yake. Aliongeza kwamba kipato duni anachotegemea hakimwezeshi kukidhi matakwa ya mtoto huyo kwani yeye hutegemea kufua nguo katika kituo kidogo cha kibiashara cha Kanyangi ili kutimiza mahitaji yake ya kinyumbani.

kiongozi wa upande wa mashtaka Murithi Mutegi aliiambia mahakama kwamba Kwamboka alijifungua mtoto huyo tarehe 3 Desemba 2017 .

Facebook Comments