Pigo Kubwa Kwa Kitili Baada ya Mahakama Kuu ya Kitui Kuagiza alipe faini ya Shilingi 100,000.

0
2184

Mahakana ya Juu mjini Kitui kumpiga faini ya laki moja Shadrack Kitili. Hii ni baada ya kesi aliyowasilisha katika mahakama hiyo kutupiliwa mbali.

Kulingana na mahakama hiyo, Shadrack Mutuku Kitili aliwasilisha kesi hiyo tarehe 26/09/2017 akipinga kutuleuliwa kwa Bi. Josephine Mutie pamoja na Bi. Florence Singi na chama cha NARC kinachoongozwa na Gavana wa gatuzi la Kitui Bi. Charity Kaluki Ngilu.

Kitili alichukua hatua ya kushtaki tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC,chama cha NARC,bunge la Kitui,Karani wa bunge la Kitui pamoja na Wawakilishi Wadi teule 15 katika bunge hilo baada ya kutoteuliwa kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Aliichukua hatua hiyo baada ya chama cha NARC kukosa kumteua katika orodha ya Wawakilishi Wadi teule kuwakilisha walemavu katika eneo bunge la Kitui Magharibi. Aidha Kitili aliteta kwamba uteuzi wa Bi Mutie na Bi.Singi kwamba ni ukiukaji mkubwa wa katiba kwani unadhihirisha ubaguzi kwa walemavu sawa na kutozingatia usawa wa kimaeneo na kijinsia.

Licha ya hayo,Kitili aliitaka mahakama kuzuia gazeti la Serikali kuwa likichapisha majina ya viongozi waliochaguliwa na wale teule akilishutumu kwa kutozingatia haki na usawa jambo ambalo lilipingwa na mahakama hiyo. Jaji Bi.Liliane Mutende alitupilia mbali ombi la Kitili na kuwagiza kulipa faini hiyo.

Jaji huyo aliongeza kwamba kesi hiyo iliwasilishwa ikiwa imechelewa sana na kwamba hakuwa na hukumu kisheria ya kuiendeleza.Katika ushahidi wake uliokuwa umeandikwa, Kitili alisema jina lake lilikuwa limechapishwa katika orodha ya Wawakilishi Wadi teule katika gazeti la kila siku la The Standard tarehe 23/08/2017 ilhali halikuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali The Kenya Gazette tarehe 28/08/2017.

Kwa sasa Kitili atalipa faini ya shilingi laki moja ambapo IEBC shilingi 50,000, bunge na Karani wa bunge la kitui shilingi 22,000 nao wabunge teule kutengewa kima cha shilingi 28,000 wagawane.

Facebook Comments