Serikali ya Kitui kuwapa mafunzo Wahudumu wa Boda Boda.

  0
  1482

  Alhamisi 11 Januari 2017, Waziri wa Elimu, Teknolojia na Masuala ya Vijana katika gatuzi la Kitui Mheshimiwa David Kivoto alikutana na waendesha bodaboda kutoka wilaya ya Mwingi ya Kati. Mkutano huo uliandaliwa katika mkahawa wa Summer Springs ulioko mjini Mwingi.

  Pia katika mkutano huo walikuwa Msaidizi wa Gavana Bwana Eric Ngilu, Mwenyekiti wa Muungano wa Wana-rika wa Kitui Bwana Moses Munyalo pamoja na mfanyi biashara tajika Julius Muinde Mutukaa.

  Serikali ya gatuzi la Kitui imeanzisha mipango ya kuandaa mikutano na waendesha bodaboda kote jimboni. Hili laja wiki chache baada ya serikali hiyo kutangaza kuwapa mafunzo vijana hao pamoja na kuwakabidhi leseni za kuhudumu barabarani katika kaunti hiyo.

  Aidha,mpango huo unanuia kuwawezesha vijana hao kujiunga pamoja katika vikundi mbalimbali zitakazowawezesha kuinua kipato chao hivyo basi kuinua kiwango chao cha maisha ya kila siku.

  Kivoto alisema kwamba uteuzi wa watakaopata mafunzo hayo utaendeshwa kwa njia ya haki na usawa katika wilaya zote 8 za kaunti ya Kitui.

  Watakaoteuliwa watapata mafunzo bila malipo pamoja na kukabidhiwa vyeti vya kuhudumu barabarani ili kufanikisha manifesto ya Ngilu ya kushughulikia masuala ya Vijana kupata kukidhi maisha yao.

  Facebook Comments