Kitui Magharibi: Kitili Mwendwa kutoa Wito wa Siasa za Amani.

0
2231

Wito wa kuendeleza siasa za amani na utulivu kutolewa na mmoja anayewania kiti cha ubunge Kitui Magharibi Maluki Kitili Mwendwa. Alikuwa akizungumza na wanahabari mjini Kitui ambapo ameahidi kuwa katika mstari wa mbele kuhimiza amani wakati huu wa kampeni kabla ya uchaguzi mdogo kufanyika tarehe 26 Januari, 2018.

Kitili anapanga kuwania wadhifa huo wa ubunge akitumia chama cha Wiper kinachoongozwa na Mheshimiwa Kalonzo Musyoka. Pia,alitoa wito wa umoja ili kuhakikisha kwamba wakaazi wa Kitui Magharibi hawapati athara mbaya kutokana na kuwepo kwa siasa mbaya.Aliomba muungano wa wanasiasa wote wa eneo bunge hilo ili kulikomboa haraka iwezekanavyo kimaendeleo.

Kiti hicho kiliachwa wazi baada ya kifo cha Mheshimiwa Francis Mwanzia Nyenze mwishoni mwa mwaka uliopita.Nyenze awali aliteuliwa na chama cha Wiper kuwa kiongozi wa wachache katika Bunge la Kitaifa baada ya uchaguzi wa 4 Machi, 2013.Mheshimiwa Nyenze alikuwa amelihudumia eneo bunge hilo kwa mihula miwili ya miaka kumi na aliaga miezi michache baada ya kuapishwa kwa muhula wake wa tatu. Aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka wa 1997 .

Spika wa bunge la Kitaifa Mheshimiwa Justin Muturi alitangaza kiti hicho kuwa wazi na kuwaomba wanaokimezea mate wajitokeze. Kulingana na katiba ya Kenya, uchaguzi mdogo yafaa ufanywe baada ya siku 90 tangu kiti kutangazwa wazi na Spika.Uchaguzi mdogo watarajiwa kufanyika 26/03/2018 kama ilivyotangazwa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Zaidi ya wawaniaji 10 kwa sasa wameonyesha hamu ya kiti akiwemo mjane wa Nyenze,Vethi Nyenze.

Isitoshe,familia ya kiongozi tajika wa Ukamba enzi za kale Chifu Kivoi Mwendwa haijaachwa nyuma katika kukimezea mate kiti hicho.Mmoja kutoka ukoo wa kiongozi huyo wa Wakamba kwa jina Maluki Kitili Mwendwa amejitosa katika kinyang’anyiro hicho cha kutafuta kuwakilisha Kitui Magharibi katika Bunge Kuu la Kitaifa la Kenya.

Facebook Comments