Mizozo baina ya Wanyama pori na Binadamu kudhibitiwa katika kaunti ya Makueni

0
2325

Shirika lisilo la kiserikali na ambalo linajihusisha na uhifadhi wa wanyama pori la David and Shedrick litatumia takriban shilingi milioni 33  kuweka ua la umbali wa kilomita 22 kwenye mbuga ya Kyulu kwenye kaunti ya Makueni kama njia moja ya kupunguza mzozo baina ya wanyama pori na binadamu.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa shilrika hili, James Mbuthia, mradi huu wa kuweka ua hiyo utaanza katika eneo la Kikunduku hadi eneo la Kithakakai kuwadhibiti ndovu ambao wamekuwa wakiwasumbua wenyeji kwenye eneo hilo huku zaidi ya vijana kumi na nane wakitarajiwa kunufaika na ajira kutokana na mradi huo.

” Hii sehemu ambayo tumedhamiria kufunga ua saa hizi ni  kilomiya 22. Wiki ijayo, tutagharamika takriban milioni moja unusu kwa kila kilomita na wal wanaoishi karibu na mbuga hiyo ndio watakaohusishwa kama kupata ajira katika mradi huo.” Bw. Mbuthia alisema.

Akizungumza na wanahabari wakati wa kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo, Bw. Mbuthia alisisitiza kuwa mbuga na mlima wa Kyulu ndio chemichemi ya maji kwenye kaunti hiyo na washikadau wote wanabidika kuhifadhi rasilimali hiyo.

ALSO READ:  Kitui's Wakili Nzamba Kitonga is dead

 

Facebook Comments