Nimechoshwa na taifa la Kenya.

  0
  1759

  Na Linah Musangi.

  Kungekua na mahali m-badala pa kuenda,ningeenda nikikimbia. Singefikiria kurudi tena.Ningekuwa na chochote ninachohitaji,” alilaumu Patrick Mathina kwa hasira.

  Mathina alizaliwa mwaka wa 1990 katika kitongoji duni cha Syomikuku katika gatuzi la Kitui.Yeye ni kifungua mimba katika familia yao ya watoto saba.

  Patrick alijiunga na shule moja ya msingi iliyo karibu na kwao na kuhitimu katika darasa la nane licha ya changamoto mbalimbali alizokumbana nazo katika safari yake ya elimu. Alipofikisha umri wa miaka 14 alikuwa tayari tegemeo la maisha katika familia hiyo yao.

  Patrick Mathina alilazimika kujitahidi kikamilifu kumsaidia mamake kutafuta kilaji cha kila siku baada ya babake kudhoofika na kulemaza baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani.

  Alianza biashara ya kusambaza maji katika hoteli zilizoko katika vituo vya kibiashara karibu na nyumbani kwao.Hili lilimwezesha kupata hela za kununua chakula cha kila siku ili kuilisha familia yao nzima. Hata hivyo, hamu na kiu yake ya elimu ilikuwa bado ingalipo.

  Baada ya miaka kadhaa ya taabu na mahangaiko,ami yake Bwana Muli alirejea nyumbani kutoka Marekani.Aliwasili katika boma lao na gari la kifahari aina ya Mercedes Benz lililokuwa na rangi ya kijivu.

  Baadaye Patrick alirudi masomoni na baada ya miaka michache alihitimu na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta.Hili lilimpa matumaini ya kufanya kazi katika ofisi kubwa hapa nchini Kenya.

  La kushangaza ni kwamba msomi Patrick alipuuza na kudharau kazi ndogo ndogo kama vile kuhudumu katika duka la M-Pesa licha ya kuwepo kwa wingi. Hizi aliziona kuwa za kiwango cha chini zaidi na zisizofaa kwa msomi kama yeye.

  Baada ya ngoja ngoja za msomi Patrick Mathina kuumiza matumbo na kuipoteza imani na matumaini ya kuajiriwa katika ofisi ya kifahari,alibadili mawazo na nia zake na kuamua kukifanya kibarua chochote mradi angepata fedha za kuikimu familia yao.

  Kwa wakati huo wazazi wake wawili walikua wameshaiaga dunia na kubaki na dada zake 6. Alijiingiza katika biashara tofauti zikiwemo kuuza mayai ya kuchemsha,aiskrimu na pia kuchoma mahindi bila ya kujali kuchomwa na miale mikali ya jua.

  Facebook Comments