Mahakama Kuu Kusitisha marufuku ya safari za usiku.

0
1649

Mahakama Kuu ilisitisha kwa muda marufuku iliyokuwa imewekewa magari ya usafiri wa umma ya masafa marefu.Marufuku hiyo ilitangazwa na almashauri ya Usalama na Uchukuzi wa barabarani hapa Kenya National Transport and Safety Authority, NTSA mwishoni wa mwaka uliopita kutokana na ongezeko la ajali za barabarani.

Mwanaharakati Okiya Omtatah alienda mahakamani kushtaki NTSA kwa kutangaza marufuku hiyo dhidi ya magari ya uchukuzi wa umma ya masafa marefu kwani ilitangazwa kinyume cha sheria na ni ukiukaji mkubwa wa katiba.Marufuku hiyo ilitangazwa 31 Desemba,2017 na na hasa iliathiri magari ya uchukuzi wa umma ya masafa marefu.

Omtata pia aliteta kwamba serikali ya Kenya haikuchukua hatua zozote kuwafidia hasara kubwa wahudumu wa matatu walizopata kutokana na marufuku hiyo.Aidha,aliongeza kwamba marufuku hiyo haina msingi wowote na haikufaa kuchukuliwa.

Jaji Chacha Mwita alitangaza kusitishwa kwa marufuku hiyo kwa kipindi cha muda usiojulikana.

Jumatano 17 Januari,2018, Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi wa Umma Paul Maringa alitangaza marufuku hiyo ingeondolewa kwa muda kuanzia katikati ya mwezi wa Februari mwaka huu.

ALSO READ:  List of 16 water projects in Nuu ward courtesy of Mbee Nzei leadership

Akiongea na wanahabari katika majengo ya Bunge alipokuwa amefika mbele ya Kamati ya Uchukuzi wa Umma, Katibu Maringa alisema kwamba miungano ya matatu italazimika kutimiza masharti ambayo yamewekwa na wizara ya Uchukuzi wa Umma kabla ya marufuku hiyo kuondolewa.

Facebook Comments