Makueni: Kizaazaa kuzuka katika mahakama ya Makindu.

0
2412

Kizaazaa kuzuka katika mahakama ya Makindu Jumatano 17 Januari, 2018 baada ya mwanamke mmoja kuomba mahakama hiyo kumruhusu kuendeleza ushirikina dhidi ya mshukiwa aliyebaka bintiye .

Mshukiwa huyo kwa jina Dominic Musyoka anakabiliwa na kesi ya ubakaji wa msichana mwenye umri mdogo. Yasemekana kwamba Musyoka alitekeleza kitendo hicho cha kubaka bintiye mwenye umri wa miaka kumi mkesha wa kuamkia siku ya wapendanao katika soko la Machinery.

Kulingana na taarifa kutoka kwa msajili wa mahakama hiyo, mshukiwa huyo hufunza katika shule moja ya upili iliyo katika eneo hilo la Makindu. Mshukiwa huyo yasemekana alimhandaa msichana huyo wa shule kwa kumnunulia chupa ya soda na hapo baadaye kumtendea tendo hilo la kinyama.

Licha ya mwalimu huyo kumwambia anyamazie kisa hicho ,alikisimulia mamake mzazi siku iliyofuata jambo lililomkera sana mamake na kuamua kumchukulia hatua kali za kisheria mwalimu huyo na kumshtaki mahakamani.

Mshukiwa huyo aliachiliwa huru na korti hiyo ya Makindu kwa bondi ya shilingi laki mbili.

Hakimu Gerald Mutiso alilazimika kusitisha na kuhairisha kusikizwa kwa kesi hiyo kutokana na ukosefu wa ripoti ya uchunguzi wa daktari. Ukosefu wa taarifa hizo za uchunguzi kamili wa daktari zilisababisha tashwishi baina mshtaki na mshtakiwa.

Mshukiwa huyo alilalamikia muda mwingi uliochukuliwa na mahakama hiyo kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu kesi hiyo ilhali mama alilalamikia kutopata haki katika kesi hiyo. Jaji Mutiso alisema kesi hiyo imehaurishwa kwa mara ya mwisho. Hiyo ilikuwa mara ya tatu kuhairishwa.

Jaji Mutiso aliamuru kesi hiyo kusikizwa tena tarehe 4/03/2017 na uamuzi wa mwisho kutolewa hapo baadaye siku hiyo.

Facebook Comments