Onyo Kali Kutolewa dhidi ya uharibifu wa mali ya umma Machakos.

0
1823

Naibu Gavana wa Machakos Francis Wambua Maliti kutoa onyo kali dhidi ya wote wanaolemaza na kutatiza miradi ya maendeleo inayoendelezwa na serikali ya gatuzi la Masaku Jumatano 17Januari,2018.

Mheshimiwa Maliti aliongeza kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayepatikana akitatiza shughuli za maendeleo kwa mwananchi zinazoendelezwa na serikali ya gatuzi la Masaku.

Alisema hayo alipozuru kijiji cha Ivumbuni wadi ya Matuu katika jimbo-ndogo la Yata. Naibu-Gavana huyo alikuwa amezuru wilaya hiyo kuzindua mradi wa maji uliofadhiliwa na serikali ya Machakos.Kisima hicho kinatarajiwa kusambaza maji kwa zaidi ya familia 300.

Mhandisi Maliti aliongeza kuwa kuna kikundi fulani cha watu ambacho kimekuwa kiking’oa na kuharibu mitambo ya jopo nishati ya jua (sola ) ambazo zinatumika kusambaza maji. Wizi wa mitambo hiyo ya sola umekuwa ukifanya wakaazi wengi wa Yata wanaotegemea kisima hicho kukosa maji safi ya kunywa na ya matumizi ya kinyumbani.

Aidha, Maliti alitahadharisha kwamba serikali ya Kaunti ya Masaku imefahamisha na kuajiri maafisa fulani kufanya uchunguzi kuwanasa wahuni wanaojihusisha katika kutekeleza uharibifu huo ili kuwanasa.Hili litawasaidia kuwachukulia hatua kali za kisheria watakaopatikana na hatia ya kuvunja mali ya jimbo.

Naibu-Gavana huyo pia alisema kwamba mali hiyo imenunuliwa na ushuru unaotozwa kwa wakaazi wa Machakos.Hivyo basi ni hatia kuharibu mali ya umma kwani wanastahili kupata huduma kwa usawa na uwazi.

Facebook Comments