Maneno ya Hekima kwa Wanawake.

  0
  3657

  Ushirikiano ni kiungo muhimu cha kujenga na kuleta umoja ili ndoa ifaulu kikamilifu.Kila mwanandoa anastahili kuhakikisha ameyatekeleza majukumu yake kikamilifu na ipasavyo.

  Mwanamke kupaaza sauti yake anapozungumza na bwanake.Hili ni tendo la kumdhalalisha na kumtweza bwana.Jambo hili hudhihirisha ukosefu wa heshima kwa mume.

  Mwanamke mwema hafai kuzitoa nje siri za ndoa yao.Anafaa kuzilinda kwa namna yoyote ile zisije kujulikana na yeyote nje ya familia na ndoa yao.Udhaifu wa mume katika ndoa haufai kujulikana na watu wengine isipokuwa bibi peke yake.Wanandoa wanastahili kulinda na kuhifadhi kikamilifu siri zao.Waama,kila mwanandoa anastahili kuwa mlinzi wa mwenzake.

  Mwanamke haruhusiwi kutumia lugha ya ishara,mitazamo na hali ili kumjulisha mumewe jambo fulani.Hili ni kwa sababu tafsiri ya mume kuhusu matumizi ya lugha ya hali na mitazamo ya mke kama njia ya mazungumzo yaweza kuwa tofauti kabisa na aliyokusudia mkewe.Wanawake wenye kujihami katika ndoa husababisha kukosekana kwa amani na utulivu katika ndoa zao.

  Mwanake hafai kumlinganisha mumeo na wanaume wenzake.Hii ni kwa maana jinsi wanavyoishi na kutamani maisha yao yawe ni tofauti na jinsi mwanaume mwengine anavyokusudia maisha yake kuwa.Mapenzi ya mume kwa mkeo yanaweza kupunguzwa na hisabu za bibi kwa mumeo.

  Bibi hastahili kuwa na mtazamo mbaya kwa marafiki wa mume wake.Mwanaume ndiye anayefaaa kujitenganisha na marafiki zake ila si mke wake.Hii ni kwa sababu hilo litadhihirisha mwanamke kutomheshimu mume wake iwapo atajitwika jukumu la kulitekeleza.

  Mwanamke anastahili kufahamu majukumu yake katika ndoa.Mwanamke aliolewa na mume ila si yeye aliyemuoa mume wake hivyo basi haja ya kudumisha heshima baina yao.Hili litachangia pakubwa kuwepo kwa amani katika ndoa.

  Mwanamke ndiye anayefaa kuwa mlinzi wa mumeo ila si mwengine.Kila mwanamke ametwikwa jukumu ka kuhakikisha ameshughulikia mahitaji ya mume wake kikamilifu.

  Hivyo basi kila mwanamke anafaa kumhughulikia mume wake ipasavyo.
  Mwanamke mwema hastahili kumlaumu mumeo ajapo nyumbani kutoka kazini mikono mitupu.Licha ya kumpuuza,mwanamke anafaa kumtia moyo mumeo.

  Usikue mwanamke wa kuketa fujo kila mara katika ndoa.Mwanamke anastahili kuwajibikia jasho la mumeo kikamilifu.

  Mwishowe ni jukumu la kila mwanandoa kufurahia matunda ya ndoa yao.Mwanamke anastahili kutimiza mahitaji ya mkewe kikamilifu ili ndoa yao idumu .Amani na utulivu katika ndoa haziji peke yake ila hutokana na yshirikiano mwema baina ya wanandoa eawili kwa pamoja.

  Facebook Comments