Serikali ya Kitui kuamrishwa kufutilia mbali marufuku ya makaa na changarawe.

0
1771

Serikali ya jimbo la Kitui kupatiwa makataa ya masaa 24 kufutilia mbali amri iliyotangaza ikiharamisha biashara ya makaa na changarawe katika gatuzi hilo.

Maneno hayo yamesemwa na Mbunge wa Kitui Mashariki Mheshimiwa Nimrod Mbai kwa ushirikiano na mwenzake wa Kitui Kusini Mheshimiwa Rachael Kaki Nyamai.
Hawa wawili wamesema kwamba marufuku hiyo haifai hata kidogo na kusisitiza kwamba wananchi wa Kitui na viongozi hawakuhusishwa ipasavyo katika kutekeleza marufuku hiyo.

Aidha , Mbai ameitaka serikali ya Kitui chini ya uongozi wa Gavana Ngilu kuondoa marufuku hiyo kwa vile imewazuia wakaazi wa Kitui kuchota changarawe ya kujenga katika boma zao na pia katika shule.

Licha ya hayo,mbunge huyo wa Mutitu amemuomba Gavana Ngilu kuandaa kikao cha dharura na wakaazi wa kitui ili kujadiliana kuhusu njia mwafaka za kulinda mazingira.Amesema kwamba watu wa Kitui hutegemea kuni na kwamba hawana budi kukata miti.Hili linasisitiza haja ya kuelimisha watu jinsi ya kupanda miti ili kujaza pengo linaloachwa baada ya kukata miti.

Maneno ya Mbai yaliungwa mkono na mwenzake wa eneo bunge la Mutomo Mheshimiwa Rachael Kaki Nyamai.Nyamai alisema kwamba kuna haja ya wabunge wote 8 wa Kitui kuandaa kikao cha pamoja ili kuwatafutia wanaotegemea biashara ya makaa njia m-badala ya kukidhi na kuendeleza mahitaji ya maisha yao iwapo marufuku hiyo itakuwa ya kudumu.

Facebook Comments