Dayosisi ya Machakos : Ndoa za familia 88 kufanyika Kaiti,Makueni.

0
8884

Jumapili ya jana tarehe 21 Januari,2018 Askofu wa Dayosisi ya Nyeri Anthony Muheria aliongoza misa ya ndoa 88 za pamoja iliyofanyika katika kanisa kuu la Parokia ya Kaumoni jimbo la Makueni katika Dayosisi ya Machakos.

Askofu wa Kanisa Katoleki kutoka Dayosisi ya Nyeri na ambaye pia anahudumu kama Askofu wa Dayosisi za Kitui na Masaku Askofu Anthony Muheria ndiye aliyeongoza misa hiyo.Hafla hiyo ilifanyika katika kanisa kuu la Parokia ya Kaumoni katika jimbo-ndogo la Kaiti gatuzi la Makueni.Familia hizo 88 zilioana kwa njia ya kitamaduni miaka ya zamani.

Akizungumza baada ya misa hiyo, Askofu Muheria aliwashauri wana-ndoa kuishi kwa amani na kusameheheana makosa yao ili kudumisha ndoa zao.Aidha ,Muheria aliwataka wapendwa kuishi Kikristo kwa kutii na kufuata kikamilufu amri kuu za ndoa.Hili litachangia kuwepo kwa umoja baina ya wapenzi katika ndoa.

Askofu aliwarai wana-ndoa kudumisha ndoa imara na kuwataka wale ambao ndoa zao ni za kitamaduni waweze kuzifanya tena kwa njia ya Kikristo.Alitaja jambo hilo la kutakasa ndoa kuwa muhimu sana baina ya Wakristo.

Pia,Askofu Muheria aliwaomba wapenzi kuwa waaminifu ili kuhakikisha ndoa zao zinadumu.Hili pia litasaidia kujenga misingi na imara ya amani na umoja baina ya wana-ndoa.Pia aliwaonya kutoka nje kuja na kuanza kuingilia ndoa zao.Hili alilitaja kuwa kinyume cha amri kuu za Dini ya Ukristo iliyoanzishwa na Mwokozi Yesu Kristo

Naibu-Gavana wa Makueni Bi. Adeline Ndeto Mwau ambaye alikuwa amefika kushuhudia ndoa hizo aliwapongeza waliochukua hatua ya kubadili ndoa zao za kitamaduni na kuzifanya katika misingi ya Ukristo.Aliwapongeza kwa kujitolea kwao na kuamua kuwa mwanga katika Parokia ya Kaumoni.

 

Mwishowe,aliwatakia kuwa na ndoa zenye amani na umoja.

Facebook Comments