Robert Leli kuikosoa hatua ya NASA na Jubilee kumpendekeza mjane wa Nyenze.

0
2449

Afueni kwa Robert Leli baada ya IEBC kuidhinisha jina lake kuwa katika orodha wagombea kiti cha ubunge cha Kitui Magharibi leo Alhamisi 25 Januari,2018.

Robert Mutiso Lili amepongeza afisa mkuu wa IEBC katika eneo bunge la Kitui Magharibi baada jina lake kuidhinishwa kuwa katika kinyang’anyiro cha kuwa mbunge .Tume huru ya Uchaguzi na mipaka Kenya IEBC ilitangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo eneo bunge hilo tarehe 26/03/2018.

Kiti hicho kiliachwa wazi baada ya kifo cha Mheshimiwa Francis Nyenze mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya kuugua ugonjwa wa saratani kwa kipindi kirefu.

Leli ameeleza matumaini yake ya kuibuka mshindi katika uchaguzi ujao.Kwa kipindi kirefu ambacho amekuwa akijihusisha na siasa hajawahi kushinda ila hujipata amebwagwa chini na wapinzani wake wakuu.

Licha ya hayo,ameelezea matumaini yake kuwa ataibuka mshindi katika uchaguzi ujao.Ameeleza kuwa atazuru kila kijiji katika eneo bunge hilo ili kuuza sera zake kwa wapiga kura ili apate uungwaji mkono na umaarufu zaidi dhidi ya wapinzani wake wakuu wa kisiasa.

ALSO READ:  2022 I will be in the ballot, Governor Malombe

Katika uchaguzi mdogo ujao wa Machi 26,2018 ,Leli atatumia chama cha NARC Kenya kinachoongozwa na Mheshimiwa Martha Karua.Alichukua hatua hiyo baada ya chama cha FORD Kenya kumpinga kuwania wadhifa licha ya kuwa tayari kufanya hivyo.

Ameongeza kwamba kila mpiga kura kutoka eneo bunge hilo yuko huru kuwania wadhifa wowote kulingana na katiba.Robert Leli aliukosoa uongozi wa eneo hilo uliopita kwa kukosa kuwahudumia wakaazi ipasavyo na kikamilifu.

Aidha,Leli amesema mbele ya hadhira kwamba alikuwa amewashinda wapinzani wake wakuu wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8,2018 .Ameapa kwamba sasa yuko tayari kutwaa ushindi katika uchaguzi ujao.

Pia amekashifu vikali viongozi kutoka ukanda wa Ukamba ambao wamekuwa wakipendekeza wagombea fulani kujitosa katika uchaguzi huo.

Facebook Comments