Historia baada ya Kitui Kusini kupata barabara ya kwanza yenye lami tangu uhuru 1963.

0
2388
Ongoing Kitui - Kibwezi road project

Ilikuwa furaha ghaya kwa Wakaazi wa eneo bunge la Kitui Kusini/Mutomo baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara kuu ya Kibwezi-Kitui.Tangu Kenya kujinyakulia Uhuru mwaka wa 1963 chini ya Waziri Mkuu ambaye pia ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa taifa letu tukufu la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Barabara kuu ya Kibwezi -Kitui ni barabara ndefu sana inayoorodheshwa kuwa ya kipekee nchini katika kiwango cha “B” ambayo inaanzia katika makutano ya barabara ya Nairobi-Mombasa katika mji wa Kibwezi,Makueni kisha inaunganisha miji mingine mikuu iliyoko katika Kaunti ya Kitui ikiwepo Ikutha,Mutomo,Kavati,Nuu na Mingwani katika kanda ya juu ya kitui kwa jina Mwingi.

Eneo bunge hilo limesalia gizani ya kupata angalau mita moja ya lami katika barabara zake hadi pale Mtukufu Rais wa jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Naibu wake H.E William Ruto walipozuru gatuzi la Kitui na kuahidi ujenzi wa barabara hiyo.Ahadi hiyo ilionekana kuwa propaganda ya serikali ya Jubilee hadi pale Rais Mtukufu Kenyatta kwa ushirikiano na Naibu wake Mtukufu William Ruto walipozindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo mwaka wa 2016.

Barabara hiyo itaunganisha pamoja maeneo bunge 8 kutoka majimbo ya Kitui na Makueni.Wiki jana ujenzi wa barabara hiyo uliweza kuvuka kutoka gatuzi la Makueni na kuingia katika gatuzi la Kitui baada ya kuvuka Mto Athi ambao uko katika mpaka wa majimbo haya mawili.Ujenzi wa barabara hiyo unakisiwa kugharimu serikali ya Jubilee kima cha Shilingi 18.4 bilioni ili kukamilika.

Serikali Kuu kupitia kwa Mbunge wa eneo hilo Mheshimiwa Rachael Nyamai imejitolea kuhakikisha ujenzi huo umekamilika haraka iwezekanavyo.Mara kwa mara mbunge huyo amekuwa akiandaa vikao na wakaazi wake ili kujadiliana kwa pamoja jinsi watakavyonufaika na ujenzi wa barabara hiyo.Kampuni la Kichina lililopatiwa zabuni ya kujenga barabara hiyo liliahidi kuwapatia ajira wakaazi wa Mutomo kwanza kabla ya kuwaajiri watu kutoka nje ya eneo bunge hilo.

Mheshimiwa Kaki akiwasiliana na watu wa Mutomo.

Mheshimiwa Rachael Nyamai alizuru eneo hilo baada ya ujenzi wa kilomita moja kukamilika katika kituo kidogo cha kibiashara cha Athi na kuekezea matumaini yake kwamba serikali kuu itaendeleza ujenzi huo hadi ukamilike.Aliongeza kwamba wafanyibiashara watakua na usafiri wa haraka kutoka Kitui na Makueni.

Licha ya hayo, Nyamai aliongeza kwamba watalii watakua na njia fupi mno kufika katika bunga la wanyama la Tsavo Mashariki kupitia upande wa Kitui na pia katika hifadhi ya wanyama pori ya Kitui Kusini ambayo inapakana na bunga kuu ya wanyama nchini Kenya ya Tsavo.

Pia usafirishaji wa madini tofauti yanayopatikana Kitui kama vile Makaa ya thamani kutoka Mui Basin,chokaa kutoka Mutomo na chuma katika Wilaya ya Ikutha utarahisishwa .

Facebook Comments