Gavana Ngilu atetea Marufuku aliyotangaza Kuharamisha Uchomaji Makaa na Biashara ya Changarawe Kitui.

0
1849

Ijumaa ya jana tarehe 09 Januari,2018 Gavana Ngilu alisema kwamba hakulenga jamii yoyote katika marufuku aliyotangaza dhidi ya uchomaji makaa na uchotaji changarawe katika mito iliyoko jimboni Kitui.

 

Gavana Ngilu alikanusha madai kwamba anailenga jamii ya Kikuyu katika marufuku aliyotangaza katika kipindi cha wiki chache zilizopita .Marufuku hiyo iliharamisha uchotaji na uuzaji wa changarawe pamoja na uchomaji makaa ya biashara katika jimbo lake la Kitui na watu ambao si wakaazi rasmi wa Kitui.

 

Hali ya maandamano ya kupinga biashara ya makaa na changarawe jimboni Kitui yamekusudiwa kwa kipindi cha siku kadhaa.Maandamano hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusisha wana-rika katika  na kufikia sasa miji tofauti iliyoko katika gatuzi la Kitui imekuwa ikishuhudia hayo.

 

Aidha,Gavana Bi. Ngilu amelazimika kujitokeza bayana na kueleza kwamba hana ufahamu wa gari lolote ambalo tayari limechomwa na kuteketezwa na wakaazi wa Kitui.

 

Gavana Ngilu alieleza wazi kwamba alilazimika kuchukua hatua ya kutangaza marufuku hiyo baada ya kuona hali ya juu ya uteketezaji wa misitu jimboni Kitui.

ALSO READ:  Kitui County Referral hospital receives medical Equipment

 

Zaidi ya hayo,Gavana aliongeza kwamba hali hiyo inachangia pakubwa ukosefu wa mvua jambo ambalo limeathiri pakubwa upatikanaji wa chakula cha kutosha.Jambo hilo linachangia pkubwa uangamizaji wa misitu na ukaukaji wa baadhi ya mito muhimu katika eneo la Ukambani.

 

Gavana Ngilu alisema kwamba kuna haja kubwa ya kulinda mazingira ili kuhakikisha uhaba wa maji umepungua.Misitu mingi imekuwa ikiangamizwa kutokana na uharibifu huo wa misitu.Wakaazi wa jimbo la Kitui wamekuwa wakilalamikia uharibifu huo mkubwa wa misitu Ukamba na uhaba wa maji katika mito iliyo katika eneo hilo.

 

Hali hii inachangia uhaba wa maji katika jimbo la Kitui.Katika habari alizotoa kwa Wanahabari Ijumaa 09 Januari,2018  Gavana Ngilu alisema kwamba takriban malori 200,000 zimekuwa zikisafirisha makaa kutoka jimbo la Kitui.

 

Ngilu alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikiharibu mazingira  kwa kiasi kikubwa.Aliahidi kwamba ataendeleza juhudi zake ili kuhakikisha ya kwamba marufuku hiyo imezaa matunda.

Facebook Comments Box