Mgombeaji Wadi kuamrishwa Kulipa faini ya 1 Milioni na Mahakama Kuu Kitui.

0
2173

Bwana Kyale Muviu adaiwa kulipa faini ya shilingi 1 Milioni kwenye Mahakama Kuu ya Kitui kwa kesi aliyopeleka kwenye mahakama hiyo kupinga ushindi wa Mheshimiwa Kivali Musyoka.

Mahakama ya Kitui leo Jumamosi tarehe 17 Februari, 2018 imetupilia mbali mashtaka yaliyopelekwa kwenye mahakama hiyo na Bwana Julius Kyale Muviu aliyekuwa akiwania nafasi ya uwakilishaji wadi ya Voo/Kyamatu eneo mbunge ya Kitui Mashariki/Mutito kaunti ya Kitui kwa kutumia tiketi ya chama cha Wiper.

Alikuwa akipinga ushindi wa Nelson Musyoka Kivali aliyeshinda kwenye kinyang’anyiro hicho kwa tiketi ya chama cha Muungano kinachoongozwa na Gavana Kibwana wa Makueni katika uchaguzi mkuu mnamo 8 Agosti,2017.

Maamuzi haya yametolewa na Jaji Johnston Munguti wa Mahakama Kuu ya Kitui leo mwendo wa asubuhi.Uamuzi huo umetolewa baada ya mahakama hii kufanya hatua ya kurudia kuhesabu kura zilizopigwa katika vitu 11 kwenye wadi hii ya Voo/Kyamatu na ambavyo Bw. Muviu alikuwa anadai kuwa kura zake kwenye vituo hivyo hazikuhesabiwa vilivyo.

Baada ya vikao vingi vya mahakama, ni makosa madogo mno ya kimsingi na yasiyokuwa nauzito unaoweza kusababisha utupiliaji mbali wa ushindi wa Bw. Kivali Musyoka.
Makosa yaliyokuwa kwenye vituo hivyo ni kuwa kura ya mpinzani ilihesabiwa na kuwekwa upande wa Bw. Kivali.

Hata baada ya kurekebisha makosa hayo Mheshimiwa Kivali bado alikua anaongoza na idadi kubwa ya kura zilizohesabiwa kwenye kinyang’anyiro hicho. Pia kura moja ya kiti cha Ugavana ilipatikana kwenye visanduku vya Mwakilisha Wadi na ambayo haikuleta utata wowote kwenye kura zao.

Hata hivyo mahakama hii imemshauri na kumpa Bw. muda wa siku 14 kukata rufaa iwapo maamuzi haya hayajamridhisha.

Facebook Comments Box