Gedion Mulyungi ashutumiwa na mkewe kuhusu mzozo wa Kinyumbani.

0
4676

Aliyekuwa Msomaji wa habari katika kituo cha televisheni cha Ebru Doreen Gatwiri amshutumu mumewe ambaye ndiye mbunge wa Mwingi ya Kati Mhesimiwa Gideon Mulyungi kuhusiana na utata na unyanyasaji wa majumbani. Gatwiri alieleza maafisa wa polisi bayana kwamba mumeo alimshambulia na kumuumiza usiku wa tarehe 26 Februari, 2018 katika boma lao lililoko mtaa wa kifahari wa Karen Jijini Nairobi.

Gatwiri aliongeza kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya kisa hicho cha kuhuzunisha kilichotekelezwa na mumewe walipokuwa katika boma lao lililoko jimboni Nairobi.Bibi huyo alipata majeraha madogo madogo kichwani mwake na katika sikio lake la kushoto jambo ambalo lilisababisha kupooza kwa sikio hilo lisiweze kusikia tena kama ilivyokuwa hapo awali.

“Naandika haya huku nikiwa na hofu na wahka mwingi. Maisha yangu kwa sasa yamo hatarini. Usiku huu mwendo wa saa 9:50 mume wangu ambaye pia ndiye Mbunge wa Mwingi ya Kati Mh. Gideon Mulyungi amenishambulia katika boma letu lililoko Karen na kuniacha na maumivu shingoni na sikioni mwangu jambo ambalo limesababisha sikio langu la kushoto kupooza,” Gatwiri aliandika mtandao wa Twitter.

 

Mke huyo aliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi kilichoko karibu na boma lao cha Hardy katika eneo hilo la Karen. Gatwiri alieleza maafisa wa polisi katika kituo hicho kwamba mumewe amekuwa akimshambulia mara kwa mara kwa kipindi cha muda mfupi uliopita jambo ambalo limetia kubwa katika ndoa yao.

Nilifanikiwa kuripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Hardy.Nahofia usalama wa maisha yangu kwa vile mume wangu amekuwa akinitishia mara kwa mara.Hii haikuwa mara yake ya kwanza ama ya pili kunishambulia na kunitishia.Nimekuwa nikinyamazia visa hivyo ili kuitunza familia na kutuliza hasira za mume wangu.Tafadhali naomba usaidizi wenu” alisema Gatwiri.

Facebook Comments Box