Familia ya Pitson,gwiji wa nyimbo za injili, yazidi kupanuka

0
3451
Photo: Pitson/Instagram

Msanii wa nyimbo za injili asambaza mtandaoni picha baada ya kubarikiwa na mtoto wa pili hivi majuzi.Ilikuwa furaha na baraka tele kwa mwimbaji Pitson baada ya mkewe kujifungua mtoto mwingine na kuwa na familia ya watoto wawili.

 

Katika mtandao wa Instagram, gwiji huyo wa nyimbo za kumsifu Yesu Kristo alisambaza picha zinazovutia za familia yake mpya.Picha zenye mnato na kuvutia ziliwafurahisha sana mashabiki wake sugu.

 

Pitson awali alikuwa mwajiriwa katika benki moja maarufu humu nchini kabla ya kugundua kipaji chake cha usanii wa nyimbo za injili.Baadaye aliziuzulu wadhifa wake na kujiunga na usanii.Baadhi ya nyimbo zake zilizovuma  na kumfanya  msanii maarufu nchini Kenya na hata katika kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati ambapo lugha ya Kiswahili  hutumika kuwasiliana ni kama vile ‘Niaje Niambie.’

Celebrated gospel singer Pitson welcomes adorable baby number two. Photo: Pitson/Instagram

Msanii huyo chipukizi alizifuatanisha picha zake na mkewe Carol Mwai na kufafanua jinsi safari ya ndoa kati yao ilivyoanzia ns jinsi imekuwa ikiendelea.Picha za malaika zilishamiri katika ujumbe wake kwa wafuasi na wazisikilizao na kuzienzi nyimbo zake.

 

Aidha,alisimulia jinsi upendo baina yake na mkewe Carol ulivyoanza miaka kadha iliyopita.Alisema kwamba kwa busu la mdomoni upendo na urafiki wao uliweza kujengeka na historia kufuatia hapo baadaye.

 

Miaka miwili iliyopita,Pitson alibarikiwa  mtoto wake wa kwanza.Kifungua mimba huyo,ambaye ni binti mrembo kupindukia,alifungua ukurasa rasmi wa maisha ya ndoa kati yake na bibiye Carol.

 

Kupitia mitandao tofauti,mashabiki wameendelea kumpongeza kwa kubarikiwa kupata mtoto mwengine.Aidha ,wengine wamefika nyumbani mwake kujionea baraka mpya kwa macho yao na kuungana pamoja na familia yake kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake mpya.

 

Kutoka Kwa: Tuko.co.ke

Facebook Comments Box