Afueni kwa Wakenya kufuatia uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za fedha kupitia rununu.

0
1968

Hivi karibuni  wateja wa mitandao ya Safaricom,Airtel na Telkom Kenya watakuwa na jambo la kujivunia  kufuatia uzinduzi rasmi wa mfumo mpya wa huduma za fedha kupitia simu zao za mikononi.

Masaibu ambayo Wakenya wamekuwa wakipitia wanapotuma na kupokea pesa kupitia simu zao za mikononi yanatarajiwa kufikia kikomo hivi karibuni kufuatia uzinduzi wa mfumo mpya wa humuma za fedha.Mfumo huo unahusisha kampuni za Safaricom, Airtel pamoja na Telkom Kenya.

Kinyume na hapo awali ambapo mteja alilazimika kutoa fedha kutoka kwa agenti wa mtandao husika ili azitume kwa mtandao mwingine, mbinu hii mpya itawezesha mteja kutuma fedha kutoka mtandao mmoja hadi mwingine bila kutozwa ada yoyote.

Hatua hiyo iliafikiwa baada ya usimamizi wa kampuni hizo tatu kuu nchini kuandaa vikao maalum ili kujadiliana kuhusu jinsi ya kukumbatia mfumo huo mpya na kurahisisha huduma za fedha.Kufikia sasa, mataifa zaidi ya 15 yamekumbatia kikamilifu mfumo huo mpya wa huduma za pesa.

Kampuni tatu kuu nchini zinazotoa huduma za mawasiliano hivi karibuni zinatarajiwa kuzindua mfumo mpya wa kutuma na kupokea fedha kwa kupitia rununu mfumo ambao unasifiwa kuwa wa manufaa zaidi kwa Wakenya.Mfumo huo utawezesha kutuma na kupokea pesa bila kujali mtandao unaotumika.Kinyume na hapo awali ambapo mmoja alilazimika kutoa pesa kwa agenti wa mtandao anaotumia pekee, mfumo huu mpya utaunganisha huduma za pesa katika mitandao yote nchini.

ALSO READ:  Nominee to the Positions of CECMs and County attorney Approved.

Usimamizi wa kampuni tatu kuu za mawasiliano nchini ulitangaza kuzindua mfumo huo ifikapo tarehe 10 Aprili, 2018 ili kurahisisha huduma za pesa.Uzinduzi huo utahusisha kampuni ya Safaricom na lile la Airtel. Telkom Kenya inatarajiwa kuzindua rasmi mfumo huo hapo baadaye.

Awali Wakenya wamekuwa wakiteta sana kutokana na kuwepo kwa mfumo changamano ambao umekuwa ukiwatoza ada ya juu zaidi wakati wanapohitaji huduma za pesa kutoka mtandao mmoja hadi mwingine.

Katika ilani iliyoandikiwa wateja wa m-pesa,airtel money na T-Kash ya Telkom,kampuni hizi zilielezea manufaa ya kuzingatia kukumbatia mfumo huo mpya wa huduna za fedha kwa wateja wao.

Kutoka kwa :Tuko.co.ke

Facebook Comments