Mtumishi kufumaniwa akishiriki ngono na ‘kondoo wake’ mjini Mwingi.

0
3482
Mutua Kasina, commonly  known as Mutume

Lilikuwa jambo la kuhuzunisha baada ya Mchungaji mmoja kuhusishwa na visa vya kuwageuza kondoo wanaoshiriki katika kanisa lake kuwa vitoweo mjini Mwingi katika jimbo la Kitui.

Kizaazaa kilizuka katika kanisa moja la kiroho mjini Mwingi baada ya Mchungaji kushambuliwa vikali na mshiriki wake kwa kumhusisha kushiriki ngono na bibiye.Imefahamika wazi kwamba Kasisi huyo anayehudumu katika kanisa la Faith Christian Church amekuwa na mazoea ya kushiriki ngono na baadhi ya kondoo wake.

Mutua Kasina,kwa jina la utani(Mutume) anashukiwa kwa kitendo cha kuwa akishiriki ngono na bibi ya mhudumu wake kwa jina John Kite.

Baada ya siku nyingi za kumshuku mkewe,mshiriki huyo kwa jina John alipanga mtego wa kutegua kitendawili hicho.Alipanga safari ya ghafla kuekekea jijini Nairobi.Mnamo Alhamisi 12-04-2018 John alimhadaa bibiye kwamba alihitajika Nairobi kwa dharura hivyo basi ilimlazimu kuondoka nyumbani.Kites alienda akajificha katika hoteli moja mjini Mwingi ili kujionea mwenendo wa bibiye.

Bila ufahamu wa yale yangemtendekea hapo baadaye,bibi huyo mrembo kupindukia alionekana katika chumba cha huduma za pesa .Hapo alitoa shilingi 500.00 kutoka kwa mhudumu huyo wa m-pesa kisha akafululiza moja kwa moja hadi kwenye kituo cha mabasi angalau apate kusafiri hadi Nairobi akapatane na ‘mpenziwe’.

Juhudi za kumzuia John kuabiri matwana hazikufua dafu hata baada yake kumuita mamaye kuja kushuhudia safari ya bintiye kuelekea jijini kumsalimia ‘mpenziwe wa dhati’.Hata hivyo,bibiye Kites alisisitiza ya kwamba hakuna yeyote aliyekuwa na uwezo wa kuikatiza safari na hivyo basi kusafiri hadi Nairobi.

Baada ya kujitumbuiza kadiri ya uwezo wao jijini Nairobi,Mutume na ‘mpenziwe’ walirejea mjini Mwingi Jumamosi tarehe 14-04-2018.

Kutokana na kupandwa na hasira kupita kiasi,John alilazimika kumshambulia Mchungaji huyo alipokuwa akiendelea kuwahudumia kondoo wake kanisani.Punde vita vilizuka baina ya wawili hao huku kasisi akimlaumu mshiriki huyo kumkashifu vikali huku akiendeleza huduma yake.

“Mutume amekuwa akishiriki mapenzi na mabibi wa wenyewe na hata wasichana wenye umri mdogo sana.Nashindwa yeye ni Mchungaji wa aina gani kutokana na kujihusisha na vichafu kama hivi.Hivi majuzi alihusishwa na bibi wa Musango,” Maria Musyoka,mmoja wa washiriki alisema.

Iliwalazimu maafisa wa polisi kutoka kituo cha Mwingi kuingilia kati baada ya malumbano kunoga na kuvuruga huduma nzima.

Wawili hao walisafirishwa hadi kituo polisi mjini Mwingi ambako wanazuiliwa hadi sasa huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukweli wa suala hilo.

Facebook Comments